MCHAKATO WA KATIBAA!! JAJI WARIOBA KUTINGA BUNGENI LEO!
Mwenyekiti wa tume ya mabadililo, Jaji Joseph Warioba anatarajiwa kufika bungeni leo kuwasilisha rasimu ya katiba kwa wajumbe wa bunge Maalum la katiba.
Mwenyekiti wa bunge hilo la latiba Samuel Sita amewaanbia wajumbe kuwepo katika bunge hilo mapema ili kuweza kusikiliza kwa makini rasimu hiyo.
Amebainisha kuwa Jaji atawasilisha rasimu hiyo kwa muda wa saa mbili, badala ya saa moja kama walivyopamga hapo awali.
Baada ya kuwasilisha rasimu hiyo watakuwa na semina ya siku tatu, Kuhusiana na rasimu hiyo, kabla ya kuanza mchakato wa kujadili rasimu hiyo ya katiba.
Ni wakati wako Mtanzania sasa kufuatilia vyombo vya habari kuweza kujua majadiliano yanavyoemdelea huko bungeni mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment